Homa ya dengue ni maambukizi ya virusi yanayoenezwa kwa kuumwa na mbu wa Aedes walioambukizwa, ambao huuma hasa wakati wa mchana. Haiambukizwi moja kwa moja kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
Ni ya kawaida katika nchi za tropiki na zilizo karibu na tropiki: karibu nusu ya watu wote duniani sasa wanaishi katika hatari, na inakadiriwa kuna maambukizi milioni 100 hadi 400 kila mwaka.
Maambukizi mengi ni madogo au hayaleti dalili zozote. Karibu mtu 1 kati ya 4 walioambukizwa huugua, na karibu 1 kati ya 20 kati ya wale wanaougua hupata dengue kali (severe dengue), ambayo inaweza kusababisha mshtuko (shock), kutokwa na damu ndani ya mwili na kifo.
Kuna aina nne za virusi vya dengue. Kuwa na aina moja hakukulindi dhidi ya nyingine, na maambukizi ya pili yana hatari kubwa zaidi ya dengue kali.

