Asidi tumboni ni jina la kila siku la dalili zinazosababishwa na asidi ya tumbo inapowasha koromeo (njia ya chakula) au utando wa ndani wa tumbo:
- Asidi kurudi kooni (acid reflux): asidi inapanda kutoka tumboni kuelekea kooni.
- Kiungulia (heartburn): hisia ya kuungua kifuani inayosababishwa na asidi hiyo kurudi.
- GERD (GORD): ugonjwa wa asidi kurudi kutoka tumboni kwenda kwenye koromeo, jina ambalo madaktari hutumia asidi inapoendelea kurudi mara kwa mara.
- Kuvimbiwa (indigestion, dyspepsia): usumbufu, kushiba kupita kiasi na kubeua baada ya kula, mara nyingi kutokana na asidi hiyohiyo.
Watu wengi hupata kiungulia au kuvimbiwa mara moja moja, na kwa kawaida si dalili ya jambo lolote zito.

